Nini cha kufanya ikiwa una ugumu wa kutimiza majukumu yako ya mkopo

Malipo kwa wakati ni jambo muhimu ikiwa umechukua mkopo. Hata hivyo, wakati mwingine hali zisizotarajiwa hutokea maishani, ambazo husababisha malipo kukoswa tarehe ya mwisho ya mkopo  au huchangia kwa hali ya kifedha na uwezo wao wa kutimiza majukumu kuwa mbaya zaidi bila kutarajia. Ni nini unaweza kufanya katika kesi kama hizo?

Punguza matumizi yako

Ikiwa umegundua kuwa kiwango chako cha mapato ya kila mwezi haitoshi kufidia gharama zako za kawaida na majukumu ya mkopo, kwanza, jaribu kutafuta njia za kupunguza gharama zako. Wakati wa kukabiliana na matatizo ya kifedha, jambo muhimu zaidi ni kuendelea na nidhamu ya kutimiza majukumu zilizotolewa na kupunguza gharama ambazo si muhimu sana kwa maisha. Kama vile:- burudani, mavazi, usafiri, n.k. Inawezekana pia kupunguza matumizi katika bidhaa za mahitaji ya msingi, kwa mfano, kwa kuchagua njia mbadala ya bei nafuu katika bidhaa mbalimbali za chakula, usafiri wa umma badala ya gari binafsi, nk.

Zungumza na taasisi ya fedha

Kuingia katika matatizo ya kifedha daima haipendezi, lakini katika hali kama hizo, lazima uwasiliane na kampuni ambayo una majukumu ya kifedha nayo. Mawasiliano kwa wakati mzuri na yanayoaminika yatakuokoa kutoka kwa ada ya kuchelewa na kuboresha uwezekano wa kufikia makubaliano na taasisi ya fedha kwa, likizo za mikopo,  malipo yaliyoahirishwa, ratiba mpya ya malipo, viwango vilivyopunguzwa, au, kwa mfano, kupunguzwa kwa malipo ya kawaida.

Fanya malipo ikiwa unaweza

Ni muhimu kufanya malipo yoyote unayoweza, hata kama taasisi yako ya fedha bado haijakubaliana na utaratibu wowote. Hii ni kwa sababu ada ya kuchelewa kawaida itaendelea kuongezeka, na ikiwa hautafanya malipo, hali yako inaweza kuwa mbaya zaidi.

Weka akiba leo

Ni muhimu kuwa na akiba ya dharura. Kuwa na pesa za ziada huweza ikakusaidia kuepuka matatizo, inaweza kuwa ni EUR 500 kukutoa kwa uguma unaopitia au gharama za maisha za miezi mitatu. Hutahitaji kukopa wakati wa shida ikiwa una pesa za kutosha katika akiba, na utaweza kulipa maswada yako bila ugumu wowote. Changamoto kubwa ni kujenga hazina yako ya dharura, ambao utakuhitaji uwe na matumizi kidogo kuliko unayopata.

Ni nini ambayo hufai kufanya

  • Usijifanye hakuna tatizo
  • Usichukue mkopo mpya kufidia majukumu ya mkopo uliopita
  • Usijaribu kuepuka mawasiliano na mkopeshaji wako

Taarifa zilizomo ndani ya chombo cha elimu wa kifedha hutolewa kwa madhumuni ya habari tu. Mtumiaji anapaswa kufanya utafiti wake kila wakati na kutafuta ushauri wa kitaalamu ili kuhakikisha kuwa mapendekezo yaliyotolewa yanafaa kwa hali yake mwenyewe. Hatuhakikishi usahihi wa jumla, ukamilifu, au kuaminika kwa ushauri wowote, maoni, taarifa, au habari nyingine iliyoonyeshwa au kusambazwa kupitia tovuti hii. Kwa hivyo, utegemezi wowote wa habari iliyotolewa ni kwa hatari yako mwenyewe.