Jinsi ya kuweka akiba na kupanga fedha za kibinafsi

Jinsi ya kuweka akiba na kupanga fedha za kibinafsi. 

Bajeti ya kibinafsi ni muhimu sana wakati wote. Hata hivyo, ina umuhimu maalum haswa wakati huu ambapo kuna dalili za kudorora, mfumuko wa bei wa haraka na upandashaji wa bei ya rasilimali za nishati katika uchumi wa dunia.  Kwa hivyo, bajeti nzuri kabisa na ambayo inaweza taabiri gharama itakusaidia kuepuka matatizo ya kifedha na kudumisha ustawi wa kiuchumi. 

Upangaji wa bajeti unaweza fafanuliwa na kanuni moja: tumia chini ya unayopata. Hata hivyo, kanuni hii hua haitumiki kila siku katika maisha yetu ya kila siku, kwa sababu kila mmoja wetu ana mahitaji yake, mazoea ya matumizi ya pesa na tamaa zetu. Wataalam huwa wanapendekeza kuwa tunastahili kuzingatia mbinu ya kina wakati tuunda bajeti.  

Hapa, utapata kanuni na sheria kuu ambazo zitasaidia kupanga fedha na gharama zako kwa mafanikio zaidi.  

Weka lengo lako.  

Tuseme umeamua kuanza kupanga bajeti yako. Kwa kawaida huwa kuna sababu yake, kwa mfano, hamu ya kupunguza matumizi ya kawaida na yasiyo ya kawaida, hamu ya kuweka akiba ili uweze kuwa na ununuzi mkubwa na mengineo. Lengo wazi, ambalo hufafanuliwa kama ahadi kwetu na ambalo huwa linatusaidia kuamua jinsi tabia zetu za matumizi zinastahili kubadilika ili tuweze kuhitimu lengo letu.  

Kuunda Mazoea. 

Kwa kawaida, tabia/mazoea yako hutengenezwa haswa kwa mda wa miezi miwili. Hapa unahitaji kuzingatia haswa nidhamu katika suala la matumizi ya fedha. Jaribu kuishi kwa uchache wakati huu na usiwe na manunuzi ya kighafla. Baada ya takriban siku sitini, utagundua kuwa kutotumia pesa ni rahisi zaidi kuliko matumizi ya pesa.  

Fuatilia Matumizi Yako. 

Wataalam hupendekeza ufuatiliaji wa pesa yako ili kuweza kuelewa fursa ya kupunguza matumizi ya pesa na kuunda tabia ya kuhifadhi pesa yako. Katika kipindi cha miezi mitatu hadi sita za mwanzo , utakuwa na fursa ya kuelewa ni gharama zipi ambazo ni za kawaida na zile zisizo za kawaida katika bajeti yako na kiasi gani unahitaji kuzipunguza. Kwa kufuatilia, inashauriwa utumie jedwali ya kina (MSExcel) au moja ya programu hizi(YNAB, Spendee, MS My Money, etc) kurekodi na kufuatilia gharama zako kwa undani na kwa kina. Hakikisha kuwa  unatenganisha gharama kwa undani uwezekanavyo, ukizingajitia gharama za chakula, usafi, Utamaduni, malazi, matumizi, vyama, sherehe, pombe, shule na elimu, mtandao, usafiri, mavazi, zawadi, mikopo, manunuzi makubwa na kadadhalika. Tathmini matumizi yako kila mwezi ili uweze kuona haswa gharama zipi unaweza punguza ili uweze kuhifadhi pesa zako.  

Zingatia Misingi. 

Gharama za msingi kwa kawaida ni zile zinazohusiana na gharama za kawaida kama malipo ya malazi, nyumba au majukumu ya kifedha kama mikopo ya benki. Hizi ni gharama ambazo muda wake wa mwsiho haupaswi kuchelewa ili kuhifadhi pesa. Wakati mwingine, chakula huwa inaongezwa kwa gharama muhimu, ambapo huwa kuna uwezekano wa kupitia/kuhakiki kikapu chako cha ununuzi na kuchagua kununa bidhaa mbadala ambazo zina bei nafuu.  

Tumia Kidogo Kwa Bidhaa Sekondari. 

Kanuni ya awali inatuongoza kwa kanuni ijayo: tumia pesa kidogo kwa bidhaa ambazo hazichangii kwa kuishi kwako. Ikiwa unataka kuhifadhi pesa, huhitaji viatu vya bei ghali au pochi la mbun. Jaribu kusawazisha, ubora wa aina, chapa, bei, na kuipa utendakazi wa bidhaa hizo kipaumbele.  

Epuka mfumuko wa bei ya Maisha. 

Mara nyingi, ikiwa kipato cha mtu kinaongezeka, matarajio yake katika matumizi ya pesa pia huongezeka – haswa manunuzi ya gharama kubwa . Hata hivyo, ikiwa kipato chako kinaongezeka, huwa haimaanishi kuwa ni lazima utumie pesa au uwe na matumizi zaidi.  

Katika kesi hii, kuna hatari ya kujiweka katika mbio za panya ambapo utaanza kupata mapato ziadi, uanze kutumia zaidi, mahitaji yako na ahadi yako ya kifedha yaanze kuongezeka, ambayo yatakulazimisha kufanya kazi kwa bidii zaidi ili uweze kupata mapato zaidi, na kadhalika.  

Utagonga mshahara na dari ya ufanisi wa kazi wakati fulani, ambayo itakulazimisha kuishi cheki kwa cheki, tena na tena. Kwa hivyo, endelea kutumia pesa zako kwa busara, ukidumisha tabia ya kuweka akiba. Huwezi kudhibiti bei ya gari, lakini unaweza kuchagua gari unaloweza kumudu. 

Usifanye maamuzi ya haraka kwa mkopo. 

Ikiwa umeimarisha kipato na matumizi yako na umefanikiwa kuweka akiba mara kwa mara, lazima utathmini kwa makini ikiwa unahitaji kuchukua mkopo ili ufanye ununuzi mkubwa au ikiwa unaweza kuweka akiba kidogo kidogo na kununua unachotaka mwenyewe. Usiharakishe kuchukua majukumu ya mikopo. Kwa kuongezea, sio kila wakati unahitaji kutumia kiwango cha juu cha mkopo kinachotolewa na benki, kwa mfano, wakati wa kununua nyumba au gari. Ikiwa umeamua kuchukua mkopo lakini unataka kudumisha tabia ya kuweka akiba, tumia muda mwingi kutathmini ofa za benki na wafadhili wengine. Zingatia ada ya utoaji wa mkopo, viwango vya riba, na gharama za ziada zinazohusiana na mkopo, na uchague chaguo la gharama ndogo. 

Weka angalau 10-20% kwenye akiba. 

Usisahau kuweka akiba zako mara kwa mara ya angalau 10-20% ya mapato yako halisi au jaribu kuunda kaushio la usalama la mishahara ya miezi mitatu au sita. Kwa njia hiyo, ikiwa utapoteza kazi yako au uwe na gharama kubwa na usiyotarajia, hautahitaji kukopa zaidi ya pesa unayoweza kulipa.  

Ni bora, kuhifadhi pesa zako kwa akaunti ambayo ni tofauti na akaunti unayotumia kufanya malipo ya kila siku kama akaunti yaani akaunti ya akiba. Wakati mwingine, unaweza pia akiba ya fedha , lakini lazima uipe makini usalama wa mahali ambapo utaweka pesa zako.  

Taarifa zilizomo ndani ya chombo cha elimu wa kifedha hutolewa kwa madhumuni ya habari tu. Mtumiaji anapaswa kufanya utafiti wake kila wakati na kutafuta ushauri wa kitaalamu ili kuhakikisha kuwa mapendekezo yaliyotolewa yanafaa kwa hali yake mwenyewe. Hatuhakikishi usahihi wa jumla, ukamilifu, au kuaminika kwa ushauri wowote, maoni, taarifa, au habari nyingine iliyoonyeshwa au kusambazwa kupitia tovuti hii. Kwa hivyo, utegemezi wowote wa habari iliyotolewa ni kwa hatari yako mwenyewe.